

Lugha Nyingine
政务要闻--江西频道--人民网
VICTORIA FALLS, Zimbabwe - Miji tisa ya China imetambuliwa kuwa miji ya ardhioevu ya kimataifa jana Alhamisi kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Nchi zilizosaini Mkataba wa Ramsar wa Ardhioevu (COP15) uliofanyika katika mji wa mapumziko wa Victoria Falls nchini Zimbabwe, ikifanya jumla ya miji kama hiyo nchini China kufikia 22, idadi ya juu zaidi duniani.
Miji hiyo tisa iliyopewa cheti cha utambulisho ni Mji Chongming huko Shanghai, Mji Dali wa Mkoa wa Yunnan, Mji Fuzhou wa Mkoa wa Fujian, Mji Hangzhou wa Mkoa wa Zhejiang, Mji Jiujiang wa Mkoa wa Jiangxi, Mji Lhasa wa Mkoa unaojiendesha wa Xizang, Mji Suzhou wa Mkoa wa Jiangsu, Mji Wenzhou wa Mkoa wa Zhejiang, na Mji Yueyang wa Mkoa wa Hunan.
Johane Chenjekwa, meya wa Kasane nchini Botswana, ameipongeza China kwa kuendeleza uhifadhi wa ardhioevu, akisema kuwa Afrika inaweza kunufaika kutokana na ushirikiano na China katika usimamizi wa ardhioevu.
"Tutaona, kadiri tunavyochangamana, kile tunachoweza kujifunza kutoka kwao. Pia wana nia ya kujifunza kutokana na jinsi tunavyofanya mambo hapa, kwa hiyo ni uzoefu (mzuri) wa kuchangamana (pamoja)," amesema.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Jay Aldous, naibu katibu mkuu wa Mkataba wa Ardhioevu, amesema kuwa wakati ukuaji wa miji unaleta maendeleo halisi, kuna haja ya kuhakikisha ukuaji huo hauingiliani na uhifadhi wa ardhioevu.
“Upanuzi wa miji ambao haujapangwa au unaosimamiwa vibaya umekuwa matatizo yanayofuatiliwa duniani, ambayo yamesababisha hali ya kuvia ya ardhi oevu, kupoteza viumbe hai, kuvuruga uwiano wa ikolojia, kuongeza utoaji wa uchafuo wa gesi, kuzidisha uchafuzi wa hewa na maji, na kuongeza athari kwa mabadiliko ya tabianchi," amesema.
Amesema katika kukabiliana na changamoto hizo na kutambua umuhimu mkubwa wa miji na ardhioevu ya mijini, Mkataba wa Ardhioevu ulizindua mpango wa kutambua Mji wa ardhioevu ili kuhimiza ulinzi wa ardhioevu za mijini na kuziweka kwenye mipango endelevu ya miji.
Mkutano huo utafungwa Julai 31, ambapo chini ya kaulimbiu ya "Kulinda Ardhioevu kwa Mustakabali Wetu wa Pamoja", pande mbalimbali zilizosaini mkataba huo zimekusanyika pamoja na kusisitiza ahadi za kimataifa za ulinzi wa ardhioevu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma